Skip to main content

Ban afurahishwa na utulivu Bangladesh

Ban afurahishwa na utulivu Bangladesh

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa BAN Ki-Moon amekaribisha kupungua kwa machafuko nchini Bangladesh katika majuma yaliyopita.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema Bwana Ban pia amefurahishwa na uamuzi wa upinzani nchini humo kushiriki katika uchaguzi wa  mabaraza ya mji katika miji ya Dhaka na Chittagong unaotarajiwa kufanyika April 28.

Katibu Mkuu amezitaka mamlaka katika taasisi zote nyeti kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa wazi, jumuishi na wenye hadhi.

Bwana Ban amenukuliwa akisema ana matumaini vyama vya kisiasa nchini Bangladesh vitapata suluhu la tofauti zao hivi karibuni kwa maslahi ya maendeleo na utulivu endelevu wa nchi. Amesema Umoja wa Mataifa unasalia imara katika ahadi yake ya kuisaidia nchi hiyo.