Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkenya ashika hatamu ICC

Mkenya ashika hatamu ICC

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC, leo wamemchagua Jaji Fernández de Gurmendi kuwa rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu, 2015-2018. Jaji Joyce Aluoch kutoka Kenya amechaguliwa kuwa makamu wake wa kwanza, huku Jaji Kuniko Ozaki wa Japan akichaguliwa kuwa makamu wa pili wa rais wa ICC.

Taarifa ya ICC imesema ofisi ya rais huchangia pakubwa katika kutoa uongozi kwa ICC kwa ujumla, ikiongeza kuwa ofisi hiyo husaidia kuratibu viungo vingine vya mahakama na kushirikiana na Mwendesha Mashtaka Mkuu kuhusu masuala yanayowahusu wote.

Kwa mujibu wa Mkataba wa Roma, rais wa ICC ana wajibu wa kuongoza mahakama hiyo kwa njia inayofaa, ingawa wajibu huo haushirikishi Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu.