Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio ni zaidi ya burudani kwa jamii za pemebezoni Kenya

Radio ni zaidi ya burudani kwa jamii za pemebezoni Kenya

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya radio duniani leo Februari 13 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na utamaduni UNESCO Irina Bokova amesema kwamba radio ni chombo muhimu katika kuleta jamii pamoja na kwa kuhabarisha huku akisema kwamba chombo hicho hutumika kupatanisha jamii zinazozozana na zinazokabiliwa na uhasama wa kisiasa. Nchini Kenya jamii za pembezoni kwa muda mrefu zimekuwa zikishuhudia changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa uwakilishi wa mahitaji yao serikalini Je ni vipi uwepo wa radio unachangia katika maisha ya jamii hizi basi ungana na Geoffrey Onditi wa Radio washirika KBC nchini Kenya katika makala hii.