WFP yasitisha mgao wa chakula kwa wakimbizi Uganda

28 Januari 2015

Nchini Uganda, shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limetangaza kukata mgao wa chakula kwa takriban wakimbizi Laki Moja na Nusu nchini humo baada ya kupata pengo la ufadhili. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya john Kibego)

Mkurugenzi wa shirika hilo humo nchini Alice Martin Daihrou amesema wamekata 50% ya chakula kwa wakimbizi hao ambao ni karibu nusu ya takriban wakimbizi 400,000 wanaoshughulikiwa kwa sasa.

Hatua imechukuliwa wakati shirika hilo limekuwa likisaka kupigwa jeki ya dola milioni 30 za ziada ili kusimamia operesheni zake katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Hata hivyo Dahirou amesema, hatua hii haitaathiri karibu wakimbizi 140,000 waliokimbia mapigano ya Sudan Kusini na watu wenye mahitaji ya kipekee kama wenye ulemavu.

Amesema inarifiwa kuwa ikiwa shirika hilo halitapata msaada katika mwezi moja ujao, mkato huo unaweza kuendelea kwa zaidi ya miezi sita na hata kuathiri wakimbizi wapya.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter