Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wanahitaji kunusuriwa Malawi: FAO

Wakulima wanahitaji kunusuriwa Malawi: FAO

Wakulima nchini  Malawi wanahitaji msaada wa dharura wa mbegu na mifugo baada ya mafuriko kuharibu mashamba na nyumba zao hivyo kuhatarisha  usalama wa chakula limesema shirika la chakula na kilimo duniani, FAO.

Kwa mujibu wa FAO zaidi ya kaya 100,000 zimepoteza mazao na mifugo kufuatia mafuriko hayo ambapo takribani watu 170,000 walilazimika kuondoka makwao, zaidi ya 70 wakithibitihswa kufariki, huku zaidi ya 150,000 wakiwa hawajulikani walipo.

Takwimu hizi ni kutoka wilaya ya Nsanje pekee. Florence Rolle ni mwakilishi wa FAO nchini Malawi

(SAUTI ya Florence)

Kiasi cha dola milioni 16 kinahitajika ili kuwanusuru wakulima nchini humo.