Kampeni ya Kuondoa Umaskini Tanzania yazinduliwa na asasi zisizo za serikali

23 Januari 2015

Mwaka 2015 ni mwaka wa ukomo wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia na wakati wa kuzindua malengo mapya ya maendeleo endelevu ambapo kampeni ya mshikamano imezinduliwa duniani kote siku chache zilizopita na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Nchini Tanzania, mtandao wa kampeni ya kuondoa umaskini Tanzania, ambao unashirikisha zaidi ya asasi zisizo za serikali 100 nchini humo, unafuatilia utekelezaji wa sera za serikali katika kufikia malengo ya maendeleo.

Kwa mujibu wa mratibu wake, Finland Bernard, bado kuna umaskini unaokithiri katika baadhi ya sehemu Tanzania.

(Sauti ya Bernard)

Hata hivyo mtandao huo umejiunga kwenye kampeni kwa kuibua maswala matatu yanayopaswa kuangaziwa na Tanzania.

(Sauti ya Bernard)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter