Maofisa polisi Libya wapewa mafunzo juu ya haki za watoto
Maofisa hamsini wa polisi kutoka nchini Libya wamehitimu mafunzo yao juu ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji watoto mafunzo yaliyofanyika nchini Tunisia chini ya uratibu wa shirika la UNICEF.
Mafunzo hayo pia yalimulika haja ya maofisa hao kuzingatia sheria za kimataifa zinazolinda haki za mtoto na kuweka mikakati ya kuwaendeleza watoto hao.