Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukeketaji umeanza kupungua barani Afrika:UNFPA

Ukeketaji umeanza kupungua barani Afrika:UNFPA

Jamii mbalimbali barani afrika zimetajwa kupiga hatua kubwa kwenye utokomezaji wa mila ya kutahiri wanawake, hatua ambayo imepongezwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na idadi ya watu duniani UNFPA.

Matokeo hayo ambayo hadi sasa inaonyesha kuwa zaidi ya jumuiya 6,000 barani afrika zimeweka kando mila hiyo, ni matunda yaliyotokana na juhudi za pamoja baina ya mashirika ya Umoja wa Mataifa UNFPA na UNICEF ambayo yamekuwa yakiendesha kampeni na miradi mbalimbali yenye shabaya ya kutokomeza vitendo hivyo.

Suala la ukeketaji watoto wa kike na wanawake kwa ujumla ni utamaduni unaendelezwa kwenye jamii nyingi barani afrika, lakini hata hivyo UNFPA imesema kuwa kasi yake imeanza kupungua na kuna ishara ya kuendelea kupunguza zaidi.

Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yamehaidi kuendelea kuendesha kampeni za mara kwa mara kwa shabaya ya kutokomeza kabisa vitendo hivyo ambavyo tayari vimewakumba mamilioni ya wanawake duniani kote.