Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvuvi watumika kupigana na umasikini

Uvuvi wa samaki katika ziwa Victoria. Picha kutoka video ya UNIFEED.

Uvuvi watumika kupigana na umasikini

Uvuvi ni moja ya sekta muhimu katika kuwezesha familia nyingi  kujikwamua kimaisha na hata katika kuhakikisha usalama endelevu wa chakula. Ijapokuwa sekta hii ina mchango mkubwa katika jamii,  mara kwa mara jamii na wavuvi wenyewe hawaichukulii uvuvi kama kazi. Nchini Tanzania huko mkoani Tanga Richard Katuma wa radio washirika Pangani FM amemtembelea mvuvi mmoja ambaye ameelezea ni jinsi gani uvuvi umesaidia katika kukidhi mahitaji ya familia yake na ungana naye katika makala hii.