Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Virusi vya mafua ya ndege vyasambaa kwa kasi Ulaya na kuzua wasiwasi kwingineko

Vifa vya ucghunuguzi wa virusi katika maabara.(Picha ya FAO)

Virusi vya mafua ya ndege vyasambaa kwa kasi Ulaya na kuzua wasiwasi kwingineko

Kugundulika upya kwa mafua ya ndege barani Ulaya mafua ambayo yanafafana na yale yaliyogundulika mwaka uliopita huko Asia, kumezusha hali ya kitisho kwa mustakabali wa sekta ya kuku hasa katika maeneo ambayo yanauhitaji mkubwa wa bidhaa hiyo.

Kulingana na Shirika la Chakula na Kilimo FAO, kuzuka kwa homa hiyo kunaongeza hali ya sintofamu katika maeneo ambayo bidhaa hiyo inategemewa zaidi kama vile nchi zilizoko kando kando ya Bahari Nyeusi na Mashariki mwa Atlantic.Taarifa kamili na George Njogopa

(Taarifa ya George)

Hadi sasa mataifa ya Ujerumani, Uholansi na Uingereza yamathibitisha kukubwa na homa hiyo ambayo pia huwakumba ndege wa msituni. Mamlaka nchini Ujerumani imethibitisha kuwa virusi hao aina ya H5N8 wameshuhudiwa katika ndege wa mwituni.

Wakati hali ikiwa hivyo barani Ulaya, mapema mwaka huu mataifa ya China, Japan na Jamhuri ya Watu wa Korea yaliarifu juu ya kuzuka kwa mafua hayo yaliyozua kizaazaa mwaka uliopita.

Hii ni mara ya kwanza virusi hivyo vikiripotiwa kuenea kwa kasi katika nchi za Ulaya ikiwa ni kipindi kifupi yaani miezi mitatu tangu iliporipotiwa kwa mara ya kwanza  mwaka huu katika nchi za Asia.

Shirika la chakula na kilimo FAO limeikumbusha dunia kuhusiana na kitisho kinachosababishwa na virusi hivyo na kusema kuwa virusi hivyo vipo na kila wakati vinajitokeza katika mazingira mapya.