Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanasayansi kutoka Burkina Faso, Iran na Peru wapokea tuzo ya UNESCO

Tuzo ya UNESCO na Equatorial Guinea

Wanasayansi kutoka Burkina Faso, Iran na Peru wapokea tuzo ya UNESCO

Wanasayansi watatu leo wamepokea tuzo ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na serikali ya Equatorial Guinea, inayohusu Utafiti katika sayansi, na ambayo imetolewa mjini Malabo leo kwenye hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa kikanda, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova.

Wanasayansi hao, Andre Bationo waBurkina Faso, Hossein Baharvard kutokaIranna Eduardo Gotuzzo waPeru, wameokea tuzo hiyo kwa niaba ya Taasisi ya Matibabu ya Tropikali,  von Humboldt (IMT) katika Chuo Kikuu cha Cayetano Heredia, Peru.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bi Bokova amesema tuzo hiyo ni utambuzi wa mchango wa kaziyaokatika sayansi na utoaji wa ujuzi ili kuhakikisha kuwa kila mtu ana maisha bora zaidi.

Miongoni mwa viongozi waliokuwepo kwenye hafla hiyo ni marais wa Equatorial Guinea, Congo, Benin, Mauritania, Sao Tome na Principe, pamoja na rais wa Muungano wa Afrika, AU, Ould Abdel Aziz.