Mkutano wa nchi za visiwa vidogo kufufua uchumi wa São Tomé

27 Agosti 2014

Wakati mkutano wa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea (SIDS) ukikaribia kung’oa nanga mnamo Septembar mosi mwaka huu nchiniSamoa, mkutano huo utatumika pamoja na mambo mengine kufufua uchumi wa São Tomé kupitia zao la Kakao.

Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD unasema kakao ilikuwa zao muhimu kwa uchumi wa visiwa hivyo na ukanda wa Afrika magharibi kwa ujumla ambapo nchi hiyo ilikuwa msambazaji mkubwa wa zao hilo duniani kabla ya bei ya kimataifa ya zao hilo kuharibu soko nchini humo.

Lakini sasa kuna mabadiliko makubwa kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya chokoleti  zinazotokana na kakao iliyolimwa bila kutumia kemikali.

IFAD kwa kushirikiana na kampuni za kutengeneza chokoleti hizo nchini Ufaransa zimeanza kupokea Kakao kutoka moja ya viwanda nchini São Tomé.  Andrea Dupaliye ni afisa kutoka IFAD

(SAUTI ANDREA)

 Wakulima sasa wanaishi kwa kutumia rasilimali kupita kiasi. Njia wanazotumia hizo za sasa sio muafaka na endelevu’’

 Sebastiana Ndeoniz ni meneja wa programu zinazohusiana na Kakao.

(SAUTI SEBASTIAN)

Kwanza ubora wa Kakao hii ni wa kipekee. Pia nafikiri  São Tomé kwa histioria yake ni nchi nzuri ya kufanyia kazi na kujaribu kuwajenga kujiamini na utu kwa wakulima tena”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud