Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amri ya kutodhihaki ufalme Thailand ni ukiukwaji wa haki ya kujieleza

Picha@Ravina Shamdasani/OCHR

Amri ya kutodhihaki ufalme Thailand ni ukiukwaji wa haki ya kujieleza

Kamishna ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imesema kuwa kumeendelea kujitokeza kwa vitendo vya kikatili pamoja na hukumu kali zinawakabili baadhi ya wananchi wa Thailand ambao hushurutishwa kupitia sheria ya lèse majesté inayolaumiwa kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza.

Msemaji wa Kamishina hiyo Ravina Shamdasani,amesema kuwa kuwepo kwa hali hiyo kunaendelea kubinya uhuru wa maoni na kwamba hali hiyo inapaswa kupingwa.

Alisema  serikali pia iliwatia nguvuni wanafunzi wawili wanaosoma chuo kikuu kwa kushiriki mchezo ulionyesha utawala kifalme.

Alisema kuwa kukamatwa kwa wanafunzi hao kumekwenda sambamba na matukio mengine ya  kutiwa korokoroni kwa watu kadhaa akiwamo mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  Plutnarin Thanaboriboonsuk, ambaye pia alifunguliwa mashtaka mengine baada ya kutuma ujumbe wa maneno kwenye mtandao wa Facebook.