Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mladenov aonya juu ya kulengwa kwa Sunni katika jimbo la Basra

Nikolay Mladenov@Picha/UNAMI

Mladenov aonya juu ya kulengwa kwa Sunni katika jimbo la Basra

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq  Nickolay Mladenov, amesema ameshtushwa na machafuko yaliyozuka hivi karibuni ambayo yaliwalenga wananchi wa jamii ya Sunni walioko katika jimbo la Basra na kuelezea wasiwasi wake baada ya kuwepo kwa ripoti iliyonyesha kufanyika utekaji na mauwaji katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Mwanadiplomasia huyo amesema kuwa tangu kuanzia Juni 23 mwaka huu si chini ya Wasunni 19 wameuawa na wengine wa idadi hiyo wakijeruhiwa katika mashambulizi ya kupangwa yaliyolenga wakazi wa eneo hilo.

Amesema kuwa mengi ya matukio hayo hayakuwahi kuripotiwa katika vyombo vya habari lakini Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo imejiridhisha juu ya kufanyika kwa mauaji hayo.

Aidha ameitolea mwito mamlaka ya jimbo la Basra kuchukua hatua za haraka ili kuzuia kutijitokeza kwa hali kama hiyo hapo baadaye.