Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laidhinisha vizuizi dhidi ya wanamgambo wa Iraq na Syria

Wakati wa kikao cha Baraza la Usalama Agosti 15.Picha ya UM/Devra Berkowitz

Baraza la Usalama laidhinisha vizuizi dhidi ya wanamgambo wa Iraq na Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuweka vizuizi dhidi ya watu sita wanaojihusisha na makundi ya waislamu wenye msimamo mkali ya ISIL na Al-Nusra.

Katika azimio hilo wanachama wa baraza hilo wameelezea kutiwa wasiwasi sana na matokeo ya vitendo vya watu hao na msimamo wao mkali juu ya utulivu wa ukanda mzima, na hali ya kibinadamu katika nchi za Iraq na Syria, wakiongeza kwamba watu hawa wanasababisha mvutano wa kikabila au kidini.

Baraza pia limelaani vikali ukiukwaji wa haki za binadamu na wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu unaotekelezwa na  ISIL, likisisitiza kwamba ISIL ni tawi lililojitenga na kundi la Al-Qaida, kwa hiyo watu wanaofadhili kundi hilo, au wanaolisaidia katika kupata silaha, kupanga au kuajiri wafuasi, basi wataandikishwa kwenye orodha ya Al-Qaida na watawekewa vizuizi.

Hatimaye barazahilolimeziomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuzuia watu wanaotaka kusafiriSyriaauIraqkwa ajili ya kujiunda na makundi hayo.