UNHCR yaonya Sri Lanka isiendelee kufukuza waomba hifadhi

12 Agosti 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR limeeleza wasiwasi wake na hali ya watu wanaoomba hifadhi nchiniSri Lankawakati huu ambapo idadi ya wanaofukuzwa nchini inaendelea kuongezeka licha ya maombi ya jamii ya kimataifa kusitisha kitendo hicho.

Tangu Agosti Mosi mwaka huu raia 88 waPakistanwamerudishwa nyumbani ambapo kwa mujibu wa UNHCR, maishayaoyako hatarini.

UNHCR imesema, mwanzoni, waliorudishwaPakistanwalikuwa ni wanaume waliofungwa tu lakini sasa wanaoufukuzwa ni familia nzima.

Tayari wanawake 11 na watoto wanane wamefukuzwa nchini humo wakisafirishwa kwa ndege hadi hadiPakistan.

Ripoti zingine zinaonyesha kwamba familia zinatawanyika, mwanaume mmoja akiwa amefukuzwa wakati mke wake mwenye ujauzito amebakiaSri Lanka.

Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards amesema:

“Ikirudisha watu hao nyumbani kwao, seriakali ya Sri Lanka inavunja sheria ya kimataifa inayokataza kufukuza mtu aliyeomba hifadhi. Kutokana na miongozo ya UNHCR iliyopelekwa kwa serikali na taasisi mbali mbali kuhusu haki za waomba hifadhi, wafuasi wa makundi madogo ya kidini, wakiwemo wakristo, washia, na waislamu waamadiyya kutoka Pakistan huwa wanaweza kuhitaji ulinzi wa kimataifa, na maombi yao ya hifadhi yanahitaji kuangaliwa kwa makini.”  

Msemaji huyo ameongeza kuwa UNHCR inarudia wito wake kwa serikali yaSri Lankairuhusu UNHCR kutembelea wafungwa 157 kutokaAfghanistan,IrannaPakistanili kutathmini mahitajiyaona maombiyaoya kupewa hifadhi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud