Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tumieni kura zenu kuleta maendeleo endelevu: Ban

UN Photo/Evan Schneider
Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. (Picha:

Vijana tumieni kura zenu kuleta maendeleo endelevu: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwenye tukio la siku ya vijana duniani hii leo na kuzungumzia umuhimu wa afya ya akili ya vijana na vijana kutumia vyema kura zao kufikia maendeleo endelevu. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Ban alitumia hadhara hiyo kumkaribisha mgeni wake Bi. Raquelina Langa kutoka Msumbiji, msichana anayejifunza shughuli za Umoja wa Mataifa, na pia alizungumzia umuhimu wa afya ya akili ya vijana ili kuondokana na unyanyapaa wanaopata pindi wanapokuwa na tatizo hilo linaloathiri upataji wa ajira na mahusiano yao.

Katibu Mkuu akagusia ukomo wa maendeleo ya milenia mwakani na umuhimu wa vijana kusimama kidete katika kufikia maendeleo endelevu yanayogusa maishayao, hivyo akasema..

(Sauti ya Ban)

"Tumieni kura zenu, uchaguzi wenu na ubunifu wenu kufikia maendeleo endelevu ambayo ni bora kwa binadamu na sayari hii. Fuatilieni mkutano wa mabadiliko ya tabianchi nitakaoandaa mwezi Septemba hapa makao makuu. Mabadiliko ya tabianchi yatawaathiri ninyi zaidi kuliko wazee kama mimi. Niungeni mkono kuwasihi viongozi wa duni kuchukua hatua mahsusi sasa. Pazeni sauti zenu.”

Naye Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu kuhusu vijana Ahmed Alhendawi amesisitizia umuhimu wa afya ya akili kwa vijana.

(Sauti ya  Alhendawi)

"Hili ni moja ya masula muhimu sana kwani linaathiri vijana duniani kote. Vijana wako hatarini sana kukumbwa na matatizo ya afya ya akili wakati wanapobadilika kutoka utoto kwenda utu uzima. Duniani, karibu asilimia 20 ya vijana wanaathiriwa na ugonjwa wa akili kila mwaka, na changamoto kubwa ya kijamii ni unyanyapaa na ubaguzi wanaokumbana nao. "