Jopo la UM latathmini hali Somalia, Mtaalamu Nyanduga ataka usaidizi uharakishwe:

11 Agosti 2014

Wajumbe wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa pamoja na Waziri wa Mambo wa Ndani wa Somalia wametembelea mji mkuu wa jimbo la Shabelle Kati nchini Somalia ili kutathmini hali iliyopo eneo hilo kufuatia mafuriko ya mwaka jana.

Mathalani wataangalia usaidizi unaotakiwa kwenye miradi ya ujenzi mpya wa mifereji ya maji iliyoharibiwa na mafuriko hayo.

Wakati hayo yakiendelea, Bahame Tom Nyanduga, ambaye ni Mtalaam Huru wa Umoja wa Mataifa kwa Haki za Binadamu nchini Somalia, amerudia ombi la Umoja huo la dola milioni 663 ili kuzuia Somalia isiathirike tena na baa la njaa.

(Sauti Nyanduga-1)

Ameeleza kwamba hali hiyo imesababishwa na mapigano yanayoendelea dhidi ya kundi la Al-Shabab, na mvua kutonyesha vya kutosha wakati wa msimu uliopita.

Hata hivyo amesema, serikali ya Somalia inajitahidi kupambana na ugaidi na kutengeneza katiba mpya, kwa hiyo inafaa kusaidiwa:

(Sauti Nyanduga-2