Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Djinnit alaani kuibuka tena mashambulizi ya kikatili Nigeria

Uharibifu baada ya shambulizi na Boko Haram katika kituo cha polisi Kano, Nigeria.PIcha:IRIN/Aminu Abubakar(UM/News Centre/maktaba)

Djinnit alaani kuibuka tena mashambulizi ya kikatili Nigeria

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukanda wa Afrika ya Magharibi, Said Djinit, amelaani vikali mauaji ya raia yaliyoripotiwa kutekelezwa mwishoni mwa wiki na hapo jana na kundi ya kigaidi la Boko Haram kwenye mji wa Damboa, Jimbo la Borno naKaduna, jimbo laKaduna. Taarifa kamili na Amina Hassan

(Taarifa ya Amina)

Bwana Djinnit ameelezea kusikitishwa mno na mashambulizi hayo, ambayo ripoti za awali zinasema kuwa yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 130, na kulazimisha wengine wapatao 15,000 kuhamiaMaiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno na miji jirani ya Biu na Goniri.

Djinnit ametuma rambi rambi zake kwa familia za wahanga, na kuelezea mshikamano wake na wahanga na serikali yaNigeria.

Amehimiza mamlaka zaNigeriakufanya juhudi zaidi kukomesha wimbi la ukatili na kuwafikisha watekelezaji wa uhalifu huo mbele ya sheria.

Djinnit Amerejelea pia ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuunga mkono ushirikiano wa kikanda wa kuondoa tishio la ugaidi na kutokomeza mashambulizi ya Boko Haram.