Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lasikitishwa na mzozo wa Gaza

Hali ya uhai kutokana na vizingiti yanazidi kufifia Gaza na Ukanda wa Magharibi. Picha@ Shareef Sarhan/UNRWA

Baraza la Usalama lasikitishwa na mzozo wa Gaza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limeelezea kutiwa wasiwasi na tatizo la mzozo wa Gaza na ulinzi wa maisha na maslahi ya raia wa pande zote.

Wanachama wa Baraza hilo wametoa wito wa kutaka hali hiyo itulizwe na kuhshimu tena makubaliano ya kusitisha mapigano ya Novemba 2012.

Wametoa wito pia sheria ya kimataifa ya kibinadamu iheshimiwe, ukiwemo ulinzi wa raia..

Wanachama hao wa Baraza la Usalama pia wameelezea uungaji wao mkono wa kuanza tena mazungumzo ya moja kwa moja baina ya Waisraeli na Wapalestina, kwa lengo la kufikia mkataba wa kina wa amani wenye msingi wa suluhu la mataifa mawili.