Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA: watu 300 wameshajeruhiwa Gaza

@UNICEF Palestine

OCHA: watu 300 wameshajeruhiwa Gaza

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA, leo imetoa ripoti kuhusu hali ya usalama na ya kibinadamu katika maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Shirika hilo, limesema, tangu mwanzo wa operesheni za Israel kupiga mabomu dhidi ya maeneo hayo, zaidi ya watu 35 wamefariki dunia na 300 wamejeruhiwa, wakiwemo watoto, watu 900  wakilazimika kuhama makwao baada ya kubomolewa kwa nyumba zao.

Juu ya hiyo, shule 13 zimeshaharibika kwa kiasi Fulani, pamoja na kituo cha kusafisha maji machafu, ikisababisha tani milioni 25 ya maji machafu kupelekwa moja kwa moja kwenye bahari.

Ingawa chakula bado kinapatikana, Shirika la Kuwasaidia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA likiendelea kusaidia zaidi ya wakimbizi 800,000, shirika la OCHA linasema kuna mahitaji ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya familia zillizolazimika kuhama, madawa na msaada wa kisaikolojia.