Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa mafunzo Liberia kama njia ya kukabiliana na Ebola

WHO/Christina Banluta

WHO yatoa mafunzo Liberia kama njia ya kukabiliana na Ebola

Viongozi wa jamii katika wilaya tatu nchini Liberia Montserrado, Margibi, na Lofab wanapokea mafunzo kuhusu virusi vya Ebola, kama sehemu ya juhudi za Shirika la afya duniani WHO na wizara ya afya ya jamii katika kuhamasisha kuhusu ugonjwa huo, jinsi gani unaambukizwa na mchango wa umma katika kukabiliana na ugonjwa huo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya

(Taarifa ya Grace)

Mafunzo hayo yanajumuisha pia taarifa zilizochapishwa zinazosambazwa kwa watu kuhusu matibabu, vituo vya huduma na jinsi ya kuzika maiti.

Kadhalika WHO imetoa mafunzo kwa viongozi wa dini kote nchini katika eneo la New Kru mjini Monrovio. Mafunzo yaliongazia jinsi ya kujikinga dhidi ya virusi vya Ebola.

WHO imetaja umuhimu wa kutoa mafunzo kwa viongozi hawa kwa sababu ya imani na ushawishi walio nao kwa jamii na wana uwezo wa kuchangia katika watu kubadili mienendo yao kwa mfano kutafuta matibabu ili kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.