Kobler awapongeza raia wa DRC wakati wa siku ya uhuru

30 Juni 2014

Leo ikiwa ni miaka 54 ya uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa MAtaifa nchini humo, Martin Kobler, ametuma pongezi zake kwa raia wa nchi hiyo katika ujumbe uliochapishwa kwa lugha zote za kitaifa za DRC, ikiwemo Kiswahili, huku akisema, DRC si ardhi tu, bali ni raia, ni taifa, ni historia na ni hatma.

Kobler amewapongeza raia wa DRC kwa juhudi zao katika kujenga nchi yenye uhuru , akisema anashangaa na bidii, ujasiri na busara ya wananchi wao, ambao wanajituma kujenga nchi yenye amani na manufaa, akiongeza kwamba familia ya Umoja wa Mataifa itaendelea kuwasaidia.

Hatimaye, amenukuu shujaa wa uhuru wa DRC, Patrice Lumumba, akimwandikia mke wake awaambie watoto wao kuendelea kupigania uhuru wa nchi yao, kwa sababu hakuna watu huru bila nchi huru, Kobler akiongeza, na wanawake huru pia!

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter