Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti yafichua uhalifu mkubwa porini, Kenya tayari imechukua hatua

Uhai wa tembo uko mashakani, ripoti yaibua mapya. Picha@UNEP

Ripoti yafichua uhalifu mkubwa porini, Kenya tayari imechukua hatua

Ripoti mpya ya shirika la mazingira duniani, UNEP na lile la kimataifa la polisi, INTERPOL imehusisha uhalifu wa bidhaa za porini na vitendo vya kigaidi.

Ikiwa imezinduliwa leo kando mwa mkutanowa baraza la mazingira huko Nairobi, ripoti inasema zaidi ya dola Bilioni 200 zinazopatikana kwenye biashara ya pembe za ndovu, vifaru na mbao hufadhili uhalifu, vikundi vya kigaidina kutishia usalama na maendeleo duniani.

Mojawapo ya nchi zinazoathirika na ujangili wa wanyamapori ni Kenya ambapo mwakilishi wake UNEP, Balozi Martin Kimani anataja hatua walizochukua.

(Sauti ya Balozi Kimani)

Kwa mujibu wa Balozi Kimani ujangili wa wanyamapori usipodhibitiwa utaathiri sekta ya utalii ambayo inaajiri watu Laki Sita, hivyo ameomba usaidizi wa jamii ya kimataifa kutokomeza vitendo hivyo.