Ban, Pillay walaani adhabu za waandishi wa habari Misri

23 Juni 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Navi Pillay wameeleza kusikitishwa kwao na adhabu za vifungo vya miaka 7 na 10 zilizopewa kwa waandishi wa habari watatu wa Al-Jazeera, pamoja na wengine 11 ambao hawakuwepo mahakamani.

Amesema, adhabu hiyo, na vilevile ile ya jumamosi ya kuwakatia adhabu za kifo watu 183 kutoka jumuiya ya Waislamu ni aina za adhabu ambazo zinapewa katika hali ya utata wa kisheria na zinavunja sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari siku ya leo, msemaji wa KAtibu Mkuu Stephane Dujarric amesema kwamba Ban ana wasiwasi wa uamuzi huo wa hivi karibuni zaidi nchini Misri..

Katibu Mkuu anasisitiza kuwa kushiriki katika maandamano yenye amani, ama kukosoa serikali, vyote havipaswi kuwa msingi wa kukamatwa na kushikiliwa au kufungwa. Anaamini kuwa Misri itaimarika kwa kuwawezesha raia wake wote kutumia haki zao.”

Nayo taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imemkariri Bi. Pillay akisema kuwa vyombo vya habari na mashirika yasiyo ya serikali nchini Misri yanaazidi kunyanyaswa na kunymwa uhuru wao wa msingi, tabia hizo zikiwa zimegeuka kawaida, akisema ni muhimu nchi hiyo kusitisha vitendo hivyo.

Hatimaye, alikumbusha Kifungu 19 cha Mktaba wa Kimataifa kuhusu haki za kijamii na za kisiasa kuhusu haki ya kujieleza huru, akisema kubeba kamera si uhalifu, akiiomba serikali ya Misri kuwaachi huru waandhisi wote wa habari walioko magerezani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter