Idadi ya wakimbizi wa ndani Ukraine yaongezeka

20 Mei 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limesema kuwa hivi sasa kuna takriban wakimbizi elfu kumi wa ndani nchini Ukraine. Msemaji wa UNHCR, Adrian Edwards, amesema kuwa mashirika ya kimataifa na mamlaka za kitaifa zinatoa usaidizi wa huduma za sheria, pesa za matumizi na kuboresha makazi ya dharura.

Ameongeza kuwa idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao imekuwa ikipanda tangu kura ya maoni ya mwezi Machi. Watu wengi wamekuwa wakikimbia ama kwa sababu za kutishwa au usalama na mateso

Wengine wanaripoti kuwa wamepata vitisho kupitia kwa njia ya simu, mitandao ya kijamii, au kupata maandishi ya vitisho yameachwa nyumbani kwao. Watu wanataja kuhofia kuteswa kwa sababu za kikabila, imani zao za kidini, au wengine kama waandishi habari, wanaharakati wa haki za binadamu na wasomi, kwa sababu za kazi zao au taaluma zao”

Watu waliolazimika kuhama ni wale wa kabila la Tartar, lakini hivi karibuni pia watu wa asili ya Ukraine na Warusi wamekuwa wakikimbia.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter