Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho inaongezeka:Ban

Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa taasisi ya Shanghai alipokaribishwa na wakuu wa taasisi hiyo(Picha ya UM/Mark Garten)

Tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho inaongezeka:Ban

Ukosefu wa usawa unaongezeka kila uchao duniani kote halikadhalika ustahimilivu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alipozungumza kwenye taasisi ya Shanghai kuhusu masomo ya kimataifa huko China aliko ziarani kama inavyofafanua taarifa ya Alice Kariuki.

(Taarifa ya Alice)

Ban amesema ukosefu wa haki uko kila pahala na hilo linachochea ukosefu wa usalama. Mathalani amesema wanawake bado wanashindwa kupata haki sawa, vijana wanasaka matumaini na ustawi na mara nyingi wanasaka ajira.

Upatikanaji wa rasilimali za msingi kama vile nishati, chakula, ardhi, maji na hewa safi unazidi kudorora na hivyo amesema ni vyema Umoja wa Mataifa ukasimamia kidete mambo makuu matatu ambayo ni kuchagia kufikia malengo ya milenia kabla ya 2015 hususan kutokomeza njaa na umaskini kwa asilimia 50 akisifu China kwa kusaidia lengo hilo kufikiwa mapema.

Pili ametaja kipindi baada ya mwaka 2015 cha kuweka ajenda mpya akisema ni fursa ya kutokomeza umaskini. Tatu amesema ni mabadiliko ya tabianchi kwani amesema kila mtu anafahamu kile wanasayansi na umma wanaeleza kuwa athari hi dhahiri.

Amerejea wito wake wa mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi mwezi Septemba mwaka huu akitaka nchi kutoa ahadi za kufikia makubaliano mapya mwakani. Hivyo amesema anatarajia China kutoa uongozi na mawazo duniani kuelekea azma hiyo.