Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lishe duni yahatarisha afya ya umma zaidi kuliko tumbaku: Umoja wa Mataifa

Oliver de Schuter

Lishe duni yahatarisha afya ya umma zaidi kuliko tumbaku: Umoja wa Mataifa

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki ya chakula Olivier De Schutter, ametoa wito akitaka kufikiwa makubaliano mapya ya dunia kwa ajili ya kukabiliana na mienendo ya ulaji usiozingatia afya kwa maelezo kuwa uhalaji holela usiofuata kanuni ni tishio kubwa kwa afya ya binadamu kuzidi mathara yasababishwayo na tumbaku.

Taarifa kamili na George Njogopa:

Wakati duniani ikiweka mikakati ya pamoja kwa ajili ya kukabiliana na matumizi ya tumbaku, mtalaamu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuna haja kutupia macho maeneo yanayohusu ulaji usiozingatia afya.

Akizungumza mjini Geneva kuelekea kwenye kongamano la kimataifa ambalo linatazamiwa kuzindua mkakati mpya mtaalamu huyo amesisitiza dunia hajachukua hatua za kutosha.

Amesema kuwaa pamoja na madhara ya ulaji usiozingatia afya kuanza kuonyesha athari zake, lakini dunia ikiendelea kuyapa kisogo mambo hayo kana kwamba hayatokei kabisa.

Kongamano hilo la siku ya mlaji duniani linapangwa kufanyika Mei 21 kwa kuzinduliwa mpango maalumu ambao utajulikana kwa jina la “Mkakati wa kimataifa juu ya kulinda na kuendeleza ulaji unaozingatia afya.