Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yanoa watendaji wa Tume za Uchaguzi Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.

Jaji Francis Mutungi msajili wa vyama na Joram Rukambe (DEP) (Picha ya UNDP Tanzania)

UNDP yanoa watendaji wa Tume za Uchaguzi Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unaendesha mafunzo ya wiki moja kwa ajili ya maafisa 20 wa Tume ya Taifa ya uchaguzi, NEC na Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ZEC ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge utakaofanyika mwakani.

Mafunzo hayo yaitwayo BRIDGE au uwezeshaji kwa demokrasia, utawala bora na uchaguzi yanaratibiwa na kuendeshwa na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Tanzania chini ya mradi wake wa demokrasia na wahitimu wanatarajiwa kuwafundisha wenzao.

Godfrey Mulisa mratibu wa mradi huo anaeleza kwa nini wakati huu.

(Sauti ya Godfrey)

Bwana Mulisa amesema mafunzo haya ni tofauti na yale waliyotoa kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.

(Sauti ya Godfrey)

Mahojiano na Mulisa kuhusu mafunzo hayo yanayofanyika Bagamoyo, mkoani Pwani nchini Tanzania yatapatikana katika ukurasa wetu.