Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inasikitishwa na hali ya wakimbizi, serikali yaanza kuwasafirisha kuelekea makambini:Kenya

UNHCR inasikitishwa na hali ya wakimbizi, serikali yaanza kuwasafirisha kuelekea makambini:Kenya

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasikitishwa na kukamatwa na kuzuiliwa kwa takriban wakimbizi elfu moja na waomba hifadhi  waliokamatwa wakati wa operesheni ya kukabiliana na ugaidi inayotekelezwa na vikosi vya usalama  nchini Kenya mji mkuu Nairobi tangu mapema mwezi huu ikilenga wakimbizi wasio na vibali.

Wakati hali ya wakimbizi ikiwa sio nzuri serikali ya Kenya imeanza mpango wa kuwafirisha wakimbizi kuelekea kambini. Katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa Idhaa hii Abel Mbilinyi, Naibu Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini humo anaanza kwa  kueleza kile walichoshuhudia katika uwanja wa Kasarani.

(Mahojiano)