Polio yatokomezwa Kusini-Mashariki mwa Asia: WHO

27 Machi 2014

Nchi za Ukanda wa Kusini-Mashariki mwa Asia zimetangazwa rasmi kuwa zimetokomeza ugonjwa wa Polio, na hiyo ni kwa mujibu ripoti ya shirika la afya duniani WHO. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ukanda huo una nchi 11 ambazo ni Bangladesh, Bhutan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, India, Indonesia, Maldives, Myanmar, Nepal, Sri Lanka, Thailand na Timor-Leste.

WHO inasema uthibitisho wa nchi hizo kufanikiwa kutokomeza Polio una maana kuwa idadi ya watu duniani wanaoishi maeneo yasiyo na polio imeongezeka na kufimia asilimia 80.

Ijapokuwa tangazo hilo ni habari njema kwa nchi husika, WHO inaonya kuwa hazipaswi kulegeza hatua zao za kinga na udhibiti kwa kufanya uchunguzi na kuendeleza chanjo.

Nchi ambazo hadi sasa Polio inatishia uhai wa wananchi wake ni Nigeria, Afghanistan na Pakistan.

HAta hivyo hivi karibuni kumekuwepo na ripoti za mkurupuko wa polio huko Syria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Israel, Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, Gaza, Kenye na Somalia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud