Wasyria wanakabiliwa na hali ngumu na njaa

5 Machi 2014

Mamia ya wananchi wa Syria wanaripotiwa kuwa katika hali mbaya wengi wao wakiwa wamelundikana kwenye maeneo yaliyoshambuliwa na mabomu hali ambayo inazidisha wasiwasi mkubwa.

 Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti moja iliyotolewa na Kamishana moja ya. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya george)

Ripoti hiyo inasema kuwa  wamekuwa na mbinu za makusudi zinazofanywa ili raia hao wasifikiwe na huduma za dharurakamavile chakula, madawa na na wamekuwa wakiamuliwa kuchagua kati ya mambo mawili, kuendelea kutaabika na njaa ama kujisalimisha.

Kamishna hiyo imesema kuwa makundi ya wapiganaji pamoja na vikosi vya serikali ni baadhi ya makundi ambayo yameshiriki kwenye uhalifu huo ambao umeambatana na vitendo vya mauwaji, kunyonga raia bila kufuata taratibu za kimahakama na kuwaandikisha watoto kuwa askari.

Ripoti hiyo imefichua kwa mara ya kwanza kuhusika kwa makundi ya waasi kwenye vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu.

Mwenyekiti wa Kamishna hiyo Paulo Sérgio Pinheiro, amesema kuwa kushindwa kwa jumuiya za kimataifa kuchukua hatua kumezidi kuongeza hali ya wasiwasi kwa wananchi kuhusiana na mustakabala wao.

 (Sauti ya Pinheiro)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter