Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafua ya ndege yasababisha kifo kimoja China, huko Malaysia nako kisa kimoja charipotiwa

Mafua ya ndege yasababisha kifo kimoja China, huko Malaysia nako kisa kimoja charipotiwa

Nchini China homa ya mafua ya ndege isababishwayo na kirusi aina ya A(H7N9) imeendelea kuwa tishio ambapo imesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine Tisa wamethibitishwa kuambukizwa.

Shirika la Afya duniani, WHO limesema limepata uthibitisho kutoka tume ya taifa ya afya na uzazi wa mpango nchini China ambayo imesema kuwa wagonjwa hao kwenye majimbo ya Guangdong, Anhui, Hunan na Jiangsu wana umri kati ya miaka minne hadi 84.

Msemaji wa WHO Glenn Thomas amesema hali za baadhi ya wagonjwa ni mbaya na kwamba wagonjwa watatu kati ya hao wameonekana kuwa na historia ya kuhusika na kuku. Hata hivyo amesema uchunguzi unaendelea wakati huu ambapo Serikali ya Malaysia nayo imeripoti mgonjwa mmoja wa homa ya mafua ya ndege.