Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNAMID akutana na makundi ya Darfur nchini Uganda

Mkuu wa UNAMID akutana na makundi ya Darfur nchini Uganda

Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur nchini Sudan Mohamed Ibn Chambas yuko Kampala nchini Uganda ambako amekutana na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jimbo la Darfur. 

Katika ziara yake hiyo ya siku tatu, Mpatanishi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na makundi ambayo bado hajatia saini makubaliano ya pamoja na usitishwaji wa mapigano. Miongoni mwa makundi hayo ni pamoja na lile la  (SLA/AW), Sudan Liberation Army na Justice and Equality Movement . 

Shabaha kubwa ya ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji majadiliano ya pamoja yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka uliopita Addis Ababa, Ethiopia. 

Akizungumza baada ya kukutana na makundi hayo, mwanadiploamasia huyo wa UNAMID alisema kuwa ametia moyo na pande zote zilivyoonyesha ushirikiano na kuongeza kuwa hali hiyo imetoa ishara njema ya kupatikana suluhu ya kudumu katika eneo hilo lenye mzozo la Darfur.