Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yapambana na surua miongoni mwa wakimbizi wa Sudan kusini nchini Uganda

UNHCR yapambana na surua miongoni mwa wakimbizi wa Sudan kusini nchini Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo Ijumaa limeanza kampeni kubwa ya chanjo Kaskazini mwa Uganda ili kuzuia kusambaa kwa surua miongoni mwa wakimbizi wa Sudan Kusini. Flora Nducha na maelezo kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Wizara ya afya yaUgandaimethibitisha kuwepo kwa mlipuko wa surua miongoni mwa wakimbizi zaidi ya 59,000 wa Sudan Kusini ambao wamewasili nchiniUgandatangu kuzuka kwa machafuko Sudan Kusini katikati ya mwezi Desemba.

Visa vitano vimeorodheshwa hadi sasa na vingine vitatu vinashukiwa katika eneo la Arua . Vipimo vimepelekwa maabara kwenye taasisi ya uchunguzi wa virusi nchiniUganda. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

Kampeni ya chanjo itahusisha wakimbizi wote na watoto waUgandawenye umri wa chini ya miaka 15 katika wilaya za Arua na Adjumani. Katika kampeni hii UNHCR inashirikiana na shirika la kuhudumia watoto UNICEF, wizara ya afya yaUganda, Madaktari wasio na mipaka MSF na timu ya madaktari wa kimataifa.