Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India yasherehekea miaka mitatu bila Polio

India yasherehekea miaka mitatu bila Polio

Nchini India leo ni miaka mitatu tangu kisa cha mwisho cha ugonjwa wa Polio kiripotiwe nchini humo na hivyo kuashiria mafanikio makubwa ya kuutokomeza ugonjwa huo hatari. George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

 Huku ikiendelea kutegemea ripoti za uchunguzi za kimaabara za mwezi Disemba na January, shirika la afya ulimwenguni WHO linajiandaa kutamka rasmi kwamba eneo la Kusin Mashariki mwa Asia sasa ni huru kwa ugonjwa wa polio.

WHO itatoa tamkolakehilobaadaye mwezi March na kwamba hatua hiyo itakuwa na mafanikio makubwa kwa eneohilolililoandamwa na tatizo la polio.

Kwa miaka mingi WHO imekuwa ikijaribu kukabiliana na tatizo hilo bila mafanikio na ilifika wakati shirika hilo la afya ulimwenguni liliitaja India kuwa ni nchi pekee duniani ambayo polia ni ngumu kuiondosha.

Mtaalamu kutoka mpango wa kutokomeza polio.Oliver Rosenbauer anasema kuwa mafanikio yaliyojitokeza hukoIndiayatatoa soma kwa mataifa mengine yaPakistan,Afghanistan na Nigeria ambayo bado yanaandamwa na tatizo hilo

(SAUTI YA OLIVER ROSENBAUER) (TAMKA OLIVA ROSENMBAWA)

“India imefanikiwa kutekeleza kikamilifu kampeni ya chanjo.Inaendelea kuhakikisha kwamba watoto wote wanalindwa na polio na pia wanafikia na kinga nyingine na h ii imesaidia kwa kiwango kikubwa wasiathirike. Kuna baadhi ya nchi ambazo zinatajwa kuwa na tatizo sugu la polio na nchi hizo ni Nigeria, Afghanistan na Pakistan na kadri idadi ya watu inavyozidi kuongezeka katika mataifa haya kuna uwezekano wakasambaza virusi katika mataifa mengine.”