Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na WHO walaani uingiliaji wa chanjo ya polio Al-Raga Syria

UNICEF na WHO walaani uingiliaji wa chanjo ya polio Al-Raga Syria

 Wawakilishi wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la afya duniani WHO, wamelaani vikali kitendo ya kuingilia kampeni ya chanjo ya polio kwenye jimbo la Al-Raqa nchini Syria kutokana na mapigano makali miongoni mwa makundi yenye silaha.

WHO na UNICEF wanasaidia kuhakikisha kwamba kila mtoto nchiniSyriaanapata chanjo bila kujali ni kina nani na  wako wapi. Polio ni tishio kubwa kwa watoto nchiniSyriana ukanda mzima. Inasababisha ulemavu wa maisha na watoto wote wana haki ya kulindwa dhidi ya maradhi hayo.

Mapigano sio tuu yameingilia chanjo hiyo ya polio lakini pia yamezidisha madhila kwa watu waSyriahususani kwa wanawake na watoto. Mashirika hayo mawikli yametoa wito kwa pande zote kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu chanjo ya polio kuendelea na pia kuingizwa kwa misaada ya kibinadamu.