Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa Syria watoa mependekezo yao kuhusu mkutano ujao wa kimataifa

Wanawake wa Syria watoa mependekezo yao kuhusu mkutano ujao wa kimataifa

Mkutano wa siku mbili wa kuunga mkono ujumuishaji wa wanawake wa Syria katika harakati za amani Syria umemalizika mjiniGeneva, huku wanawake hao wakitoa mapendekezo muhimu kwa kile wanachotaka kuona wakati wa mkutano wa kimataifa ujao kuhusuSyria.

Katika taarifa ilotolewa mwishoni mwa mkutano huo ambao uliandaliwa na kitengo kinachoshughulikia maswala ya wanawake, UN Women na serikali ya Uholanzi, wanawake hao wametaka pande zote katika mzozo wa Syria kuvunja mipaka ya tofauti zao ili wafikie makubaliano ya kuwepo taifa lenye uhuru, demokrasia na vyama vingi, na ambalo linaheshimu haki za binadamu, zikiwemo usawa kati ya wanaume na wanawake.

Wanawake hao pia wanataka watunga sera kuheshimu kikamilifu haki ya wanawake kushiriki kisiasa katika masuala yote yanayohusu kuweka mustakhbali mpya wa taifa lao.

Wanawake hao wamesema hawawezi kukaa kimya kuhusu matukio yaliyopo nchiniSyria,kamavile vifo vya kila siku na uharibifu, utapiamlo, mamia ya maelfu ya watu kulazimika kuhama na kuenezwa kwa ghasia na ugaidi.