Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay akaribisha uamuzi wa mahakama kuu Nepal

Pillay akaribisha uamuzi wa mahakama kuu Nepal

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay amekaribisha uamuzi wa mahakama kuu ya Nepa luliotolewa tarehe mbili mwezi huu ukitaka msamaha usitolewe kwa makosa ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliotekelezwa katika miaka 10 ya vita nchini humo. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

 (TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

 Bi Pillay amesema uamuzi huo ni hatua muhimu na maendeleo makubwa kwa maelfu ya wahanga wa machafuko hayo ya ndani.

Uamuzi huo wa mahakama kuu wa kuzuia msamaha ni hatua ya kwanza katika kuelekea kuhakikisha kwamba tume ya ukweli na maridhiano haitotumika kukwepa au kuchelewesha uchunguzi na hukumu za kesi zinazohusiana na vita.

Mwaka 2013 serikali ya Nepal ilipitisha sheria ya kuanzishwa kwa tume ya ukweli na maridhiano ili kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu uliotekelezwa kati ya mwaka 1996 hadi 2006 kulipokuwa na vita vya ndani nchini humo.Watu takriban 13,000 waliuawa na wengine 1,300 walitoweka katika kipindi hicho.