Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za misaada kwa waathirika wa kimbunga Ufilipino zimekwama-OCHA

Shughuli za misaada kwa waathirika wa kimbunga Ufilipino zimekwama-OCHA

Mashirika ya kimasaada nchini Ufilipino yamesema kuwa yameanza kuingiwa na wasiwasi kutokana na kukosekana kwa fedha kwa ajili ya kuwasaidia wale walioathirika na kimbunga Typhoon Haiyan  hivi karibuni.

Kiasi cha watu milioni 4.1 waliachwa bila makazi kutokana na kimbunga hicho kilichopiga eneo la kati ya Ufilipino  Novemba 8.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA, anasema kuwa ni sehemu ndogo tu iliyopata fedha kwa ajili ya kuendesha miradi ya dharura.

Jense Learke amesema kutokana na hali hiyo kumefanya shughuli nyingi za kuimarisha makazi kwa ajili ya waathirika hao zimesimama