Ban amteua Han Seung-soo wa Jamhuri ya Korea kuwa mwakilishi wake wa kupunguza maafa.

19 Disemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Han Seung-soo wa Jamhuri yaKoreakuwa mwakilishi wake maalum wa kupunguza  maafa. Taarifa ilioyotolewa leo alhamisi na ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imesema mteule huyo akimwakilisha Katibu Mkuu atauganisha ahadi za nchi wanachama, sekta binafsi na asisi za kiraia kuhusu kusaidia kazi ya umoja huo kuhusu kupunguza maafa yanayohusiana na maji. Taarifa hiyo inasema msisitizo utawekwa katika agenda ya maendeleo endelevu baada ya 2015 na mkutano wa mkakati wa agenda hiyo wa Hyogo nchini Japan.

Bwana Han ana uzoefu wa zaidi ya miaka mitano katika masuala ya siasa na diplomasia. Alikuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Korea mwak 2008 hadi 2009 na rais wa mkutano wa 56 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2000 hadi 2002. Amewahi kuhudumu kama mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya kukuza uchumi unaojali mazingira duniani. Kadhalika mwaka 2011 hadi 2012 alikuwa mwanachama wa mjadala mkuu wa maendeleo endelevu kuelekea mkutano waRio+ 20.

Mteule huyo pia amewahi kuwa mwakailishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na ana uelewa wa kina kuhusu suala hilo na kwa sasa ni mwenyekiti wa jopo la  wataalamu wa kiwango cha juu na viongozi kuhusu maji na majanga.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter