Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama Jamhuri ya Afrika ya Kati bado tete, chakula chahitajika.

Hali ya usalama Jamhuri ya Afrika ya Kati bado tete, chakula chahitajika.

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kiutu ,OCHA linasema hali ya usalama bado si shwari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati huu ambapo zoezi la kupokonya silaha kwa vikundi vinavyomiliki silaha hizo katika mji mkuu Bangui na Bassangoa linaendelea. Inaelezwa kuwa aliyekuwa kiongozi wa kundi la Waasi wa Seleka  Mahamat Saleh ameuawa Disemba Kumi katika mapigano mjini Bangui. Kufuatia hali tete ya usalama mjini Bossangoa, majadiliano ya msaada wa ugawaji wa chakula yanaendelea kwa jamii zote huku askrai zaidi wakihitajika. Katika eneo la Bambari wasiwasi umetanda kufuatia tetesi za mapigano kati ya waasi wa zamani wa Seleka na waasi wa Balaka.