Majeraha ya uti wa mgongo ni mabaya lakini yanazuilika: WHO

2 Disemba 2013

Takribani watu Laki Tano kila mwaka duniani kote hukumbwa na magonjwa yatokanayo na majeraha kwenye uti wa mgongo ambapo wengi wao hulazimika kuishi na maumivu hayo katika maishayaoyote kutokana na ukosefu wa tiba sahihi. Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani, wHO katika kuelekea siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu tarehe tatu mwezi huu. George Njogopa na ripoti kamili.

(Ripoti ya George) 

Kulingana na ripoti ya shirika la afya duniani WHO imesema kuwa wanaume walio na umri wa kati ya miaka 20-29 ndiyo wako hatarini zaidi kukubwa na matatizo ya kupata ajali katika sehemy za uti wa mgongo.

Pia taarifa hiyo yenye kichwa cha bahari kisemacho “ Mtazamo wa kimataifa kuhusu ajali zinazosababisha athari kwenye uti wa mgongo imewataja watu wenye umri wa miaka 70 na kuendelea kuwa ni kundi jingine ambalo lipo hatarini kukubwa na tatizohilo.

Kuhusu wanawake ripoti hiyo imesema walioko hatarini ni wale wenye umri wa kati ya miaka 15-19 na kwamba kundi jingine ni wale wenye miaka 60 na kuendelea.

Ripoti hiyo inasema kuwa zaidi ya asilimia 90 ya matatizo yatokanayo na uti wa mgongo yanachangiwa na ajali za bara barani, kuanguka kusikotarajiwa na mapigano. 

Ripoti hiyo ambayo imetolewa wakati dunia ikisubiria kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu Disemba 3, imesema kuwa wengi wanaokumbwa na matatizo ya uti wa mgongo wanakumbana na maamivu makali.

WHO inasema kuwa pamoja na kwamba tatizo la uti wa mgongo linamwondolea matumaini mhusika lakini ukweli wa mambo ajali nyingi zinazosababisha kuharibika kwa uti wa mgongo zinaepukika

 Alana Officer  ni kutoka WHO na anahusika na masuala ya ulemavu

 (SAUTI YA ALANA )

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud