Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yapatiwa Euro milioni 1.1 kutekeleza miradi Puntland

IOM yapatiwa Euro milioni 1.1 kutekeleza miradi Puntland

Shirika la Kimataifa linalohisika na wahamiaji IOM, limepokea kiasi cha Euro milioni 1.1 kwa ajili ya kutekeleza mradi wake wa kukabiliana na wimbi la usafirishaji haramu watoto na unyanyasaji wa kijinsia huko Puntland, Somalia.

Mpango huo ambao unaratibiwa kwa pamoja baina ya IOM na washirika  wake unalengo la kutoa elimu kwa wananchi na kuvijengea uwezo vyombo vya maamuzi kwa ajili ya kukabiliana na wimbi hilo.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya unyanyasaji kijinsia na usafirishaji haramu watoto hali ambayo inazusha hali ya wasiwasi katika siku za usoni.