Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yachukua hatua ya kuwalinda manusura kutoka mikononi mwa wasafirishaji haramu wa watu

IOM yachukua hatua ya kuwalinda manusura kutoka mikononi mwa wasafirishaji haramu wa watu

Huku watu zaidi wakijaribu kuhama maeneo yaliyokumbwa na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na serikali ya Ufilipino na washirika wake wamekuwa wakifanya jitiha za kuwazuia wale wanaohama kutoka kwa wasafirishaji haramu wa watu na kutambua mahitaji ya watu hao.

IOM inakadiria kuwa hadi watu 5000 wanakimbia maeneo yaliyoathiriwa kila siku wakihamia miji kama Cebu na mji mkuu Manila. Kulingana na utafiti wa IOM ni kwamba kuna uhaba wa chakula, maji na usafi kwenye sehemu tofauti za mji wa Tacloban.