UNHCR yaleta matumani kwa manusura wa kimbunga Haiyan

18 Novemba 2013

Manusura wa kimbunga Hayan Evelyn Quisaba ameelezea namna alivyonusurika kifo ikiwa siku chache tu baada ya kuokolewa katika hatari ambayo imeangamiza mamia ya raia.

Evelyn mwenye umri wa miaka 53 ambaye aliokolewa kwa kupatiwa kifaa maalumu amesema kuwa hakuamini macho yake wakati aliporejeshwa nyumbani kwake San Roque na kukuta kila kitu kimekwenda na maji.

Lakini pamoja na kuelezea namna alivyoathirika na dhoruba hiyo hata hivyo anaeleza kwamba anajambo la kumtia matumaini kutokana na msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limekuwa likizisaidia baadhi ya familia kurejea katika hali ya kawaida.