Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawasaidia wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu kutoka Ulaya:

IOM yawasaidia wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu kutoka Ulaya:

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Ufaransa limezindua mradi wa kuwarejesha katika maisha ya kawaida wahanga 130 wa usafirishaji haramu wa binadamu ambao wameamua wanataka kurejea kwa hiyari katika nchi walizotoka barani Afrika, Asia na Amerika ya Kusini wakitoka katika nchi za muungano wa Ulaya. Mradi huo wa pamoja walioouita CARE una lengo la kutathimini mahitaji ya waathirika takribani 260 walioamua wanataka kurudi nyumbani kwa sasa wengi wapo Austria, Urafansa, Ureno, Hispania na Uingereza.Jumbe