Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tangazo la Israel la ujenzi wa makazi mapya litaweka njia panda suluhu ya amani:Serry

Tangazo la Israel la ujenzi wa makazi mapya litaweka njia panda suluhu ya amani:Serry

Mratibu wa Umoja wa mataifa kwa masuala ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Bwana Roberty Serry amesema amekuwa akifuatilia kwa hofu matangazo ya Israel ya ujenzi wa makazi mapya yaliyotolewa wiki chache zilizopita , ambayo anasema hayaendi sambamba na lengo la kuwa na hatma ya suluhu ya mataifa mawili. Bwana Serry amesema msimamo wa Umoja wa mataifa ni kwamba ujenzi wa makazi mapya ya walowezi ni kinyume na sheria za kimataifa na ni kikwazo kikubwa kwa amani ya Mashariki ya Kati.

Kwa sababu hiyo leo mratibu huyo amekutana katika nyakati tofauti na wapatanishi wa majadiliano ya amani wa Palestina na Israel. Katika mkutano wake na mpatanishi mkuu wa Israel Livin na maafisa wengine wa Israel anaamini kwamba uamuzi wa jana wa ujenzi wa mipango ya kujenga idadi kubwa ya makazi sasa umesitishwa. Serry amesema katika kipindi hiki nyeti ni vyema kuepuka hatua zisizostahili na kuunga mkono majadiliano ili kuhodhi fursa za kufikia suluhu ya mataifa mawili kwa manufaa ya wote Israel na Palestina.