Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yatabiri kuongezeka kwa uzalishaji wa chakual na kushuka kwa bei

FAO yatabiri kuongezeka kwa uzalishaji wa chakual na kushuka kwa bei

Bei ya vyakula inataraajiwa kushuka ikilinganishwa na miaka iliyopita hali ambayo imechangiwa na kuongezeka kwa uzalishaji hasa wa nafaka kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO. Jason Nyakundi na ripoti kamili.,

(Ripoti ya Jason)

Bei ya vyakula kuu imeshuka miaezi michache iliyopta hali ambayo imetokana na kuongezeka kwa uzalishaji na kuzua matumani kuwa huenda chakula kikawa kingi cha kuuzwa nje na cha kuhifadhiwa. Kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula mwaka huu kunatokana na uzalishaji mkubwa wa ngano nchini Urusi na zao la mahindi nchini Marekani lakini hata hiyo uzalishaji wa mchele hautakuwa mkubwa mwaka huu. Hifadhi ya nafaka duniani inatarajiwa kuongezeka mwaka 2014 kwa asilimia 13 hadi tani milioni 564 hususan nchini Marekani.

Katika kufahamu mwelekeo wa uzalishaji na bei za vyakula kwa mwaka 2014 na baadaye, mchumi mwandamizi wa FAO Abdolreza Abassian anasema..

(Sauti ya Abdolreza)