Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CERF yatoa dola milioni 5.5 kuwasaidia watu waliaothiriwa na mafuriko nchini Sudan

CERF yatoa dola milioni 5.5 kuwasaidia watu waliaothiriwa na mafuriko nchini Sudan

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetoa dola milioni 5.5 kwa huduma za binadamu kwa watu walioathiriwa na mafuriko nchini Sudan. Kwa ujumla watu 93 waliuawa ambapo pia wengine 340,000 waliathiriwa na mafuriko. Jason Nyakundi na maelezo kamili.

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Mafuriko hayo yaliyoanza kushuhudiwa mapema mwezi Agosti yamewaathiri maelfu ya watu kote nchini. Wakati wa mvua za kwanza wafanyikazi wa kujitolea, wizara za serikali , mashiriya yasiyokuwa ya kiserikali na washirika wa Umoja wa Mataifa waliofanya jitihada za kutoa huduma za dharura.

Fedha hizo zitayaendea  mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo UNICEF, UNHCR, IOM na WHO ambayo yatashirikiana na wizara za serikali kukabiliana na jangahilo. CERF hutoa misaada wakati wa majanga ya dharura pamoja na zile huduma zisizokuwa na ufadhili kote duniani.

Tayari mwaka huu CERF imetoa dola milioni 434 kuwasaidia watu walioathiriwa na majangakama hayo duniani. Msaada wa CERF kwa taifa laSudan ndio utakuwa kwa juu zaidi kutolewa  mwaka huu zikiwa ni jumla ya dola milioni 47.4 ambazoSudan itakuwa imepokea kutoka CERF mwaka huu.